Pages

Monday, March 14, 2022

Mama Diamond Azima Kelele za Kuwa Hapendi Mahusiano ya Mwanae na Zuchu

Ingawa ni muda kiasi toka kumekuwepo na gumzo mitandaoni ya tetesi za mahusiano ya mapenzi kati ya Diamond Platnumz na msanii wake Zuchu, baada ya kutoka kwa wimbo wa Mtasubiri ambao Diamond kaimba kwa kumshrikisha mwanadada huyo uliopo kwenye EP FOA ya Diamond wadau wanaona ni kama umethibitisha tetesi hizo.

Wawili hao wamezungumziwa sana kuhusu mahusiano ya mapenzi yaliyodaiwa kuwepo huku mashabiki wengi wakiamini kwamba wimbo huo umethubitiaha uwepo wa penzi.

Wadau wa mitandaoni wakawa wanadai Diamond anashindwa kujiachia kwa kipenzi chake Zuchu kwa kuweka mambo peupe kwa ajili anamuogopa mama yake almaarufu Mama Dangote kwa ajili tetesi zinadai hayapendi mahusiano hayo. 

Na tetesi hizo zikapaliliwa zaidi na kitendo cha Mama Dangote kutom follow instagram msanii huyo wa kike pekee kwenye lebo ya mwanae.

Leo jumatatu March 14 Mama Dangote amepost video ikimuonyesha Diamond na Zuchu wakiimba wimbo wa Mtasubiri ambapo wadau wa mambo wanatafsiri kama ni ameamua kukata mzizi wa fitna.

Mdau nini maoni yako je kwani kuna nongwa yoyote endapo mzazi anaingilia penzi la mwanae?

Saturday, March 12, 2022

Nuh Mziwanda Aomba Pambano la Ngumi na Shilole

Baada ya mwanadada Shilole kutamba kumtembezea kipigo mume wake wa zamani Nuh Mziwanda iwapo atazidi kumfuatilia, naye Nuhu amevunja ukimya kwa kuomba pambano na mke wake huyo wa zamani.

"Manake hapo kwanza ncheke, Mziwanda mimi au mwingine? naomba pambano viwanja vipo vingi tu nikuonyeshe show mama Ntilie. Kwanza nina hasira na wewe ulinipiga Leaders club ukijichanganya tu nakufumua vibaya sana," aliandika Nuhu

Kwenye mtandao wa instagram mara kadhaa Nuhu amekuwa akimtuhumu Shilole ambaye kwa sasa ni mke wa mpigapicha Rommy 3D, pia mwanamuziki na mfanyibiashara ya kupika chakula kuwa alikua anajihusisha na mambo ya kishirikina enzi ya penzi lao.

Friday, March 11, 2022

Kuhusu Diamond Kumuoa Zuchu Haiwezekani - Sallam

Siku ya jana kwenye uzinduzi wa EP ya Diamond Platnumz meneja wake Sallam alitoboa siri kwamba Diamond na Zuchu hawawezi kuoana kwasababu wao wanafanya biashara na Diamond ni boss wa Zuchu.

Ishu nzima ilianza hivii: Wakati Diamond alipokuwa anatumbuiza kwenye ngoma yake mpya ya Nawaza, katikati ya tukio meneja wake Bwana Salaam akasema kila mtu atoe dukuduku lake aseme anawaza nini. Ndipo kaka wa Diamond, Romy Jons akachomekea kuwa nawaza Diamond atamuoa Zuchu na ndipo Sallam akajibu kwamba haiwezekani kwasabbau yeye Diamond ni bosi na wanafanya biashara.

Skendo kwenye Ep Ya Diamond Nawaza Kutishia Ndoa Ya Lulu na Majizzo?

EP mpya ya Diamond Platnumz FOA aliyoiachia usiku wa jana kuamkia leo imeibua skendo ya kuwepo kwa clipu za mapenzi kati ya Elizabeth Michael "Lulu" na Rayvanny hali iliyopelekea maswali mengi kwa mashabiki.

Wakati huohuo Majizzo ambaye ni mume wa Lulu kafuta posts zake kwenye ukurasa wake wa instagram akizokua amemsifia mkewe huyo ikiwemo ile ya siku ya wanawake na ya anniversary ya mwaka mmoja wa ndoa yao.

"Nawaza Vanny na Eliza clip zao zikivuja, ndoa itaimarika eti au wataivunja?" hii ni vesi iliyozua gumzo.

Aidha pia kuna baadhi ya video zinazosambaa kwenye mitandao zinazoonyesha kuwepo kwa uhusiano wa karibu kati ya Lulu na Ray.

Thursday, March 10, 2022

Ufafanuzi wa Hospitali ya Muhimbili Kuhusu Kusambaa Video ya Mgonjwa Profesa Jay

Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imetolea ufafanuzi taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Joseph Haule maarufu Profesa Jay na kusema kuna video inayosambazwa na mtandao wa Mange Kimambi ikimuonesha Profesa Jay akipatiwa matibabu Muhimbili Hospitali Upanga.

Uongozi wa hospitali unatoa taarifa kuwa video hii haijarekodiwa na kusambazwa na hospitali, tumesikitishwa na tunalaani vikali kitendo hiki cha kumrekodi mgonjwa anayepigania uhai wake ICU na kuisambaza, hiki ni kiwango cha juu cha kukosa utu na maadili.

"Tunafuatilia kwa ukaribu tukio hili ili kubaini chanzo cha video hiyo ili hatua stahiki zichuliwe, wananchi endeleeni kuwa na imani na hospitali ya Muhimbili." imeeleza taarifa iliyotolewa an hosptali ya Muhimbili.