Pages

Friday, September 7, 2012

My Article for Newspaper: Jinsi ya kuchagua pafyumu



Jinsi ya kuchagua pafyumu itakayokufaa

Pafyumu inakamilisha muonekano wako. Kuchagua itakayokufaa sio rahisi, kwanza kabisa inabidi ujijue , uwe mkweli na usifuate mkumbo kuwa pafyumu fulani ndio inavuma kwa sasa. Kwa ajili tu kila mtu anatumia pafyum fulani haimaanishi pafyumu hiyo ni sahihi kwako pia. Chagua pafyumu zinazooana na kemia ya mwili wako. Watu wengi wanakuwa wagumu kuamini ila kila binadamu ana harufu ya mwili tofauti na mwingine ingawa ni binadamu wachache wenye harufu kali kiasi cha kuweza kuzinusa. Kwa kuwa hutaweza kujaribu kila pafyumu inayouzwa madukani  makala hii itakupa dondoo ya jinsi ya kuchagua sahihi.
Fahamu kuwa pafyumu ni mchanganyiko wa mafuta ya kipekee ya mimea au wanyama na aroma za kutengeneza maabara. Harufu ya pafyumu fulani ni tofauti kati ya mtu na mtu kwa ajili kemia za ngozi ya binadamu zinatofautiana.
Kabla ya kujua uchagueje pafyumu sahihi kwanza inabidi kujua muundo wa  pafyumu.

Kuna tabaka tatu katika kila pafymu . Tabaka aina ya kwanza ni lile ambalo baada ya kupuliza pafyumu ndio harufu ya kwanza kuinusa na ndio inayokuvutia. Tabaka hili halikawii kupotea na harufu inakaa kati ya dakika 10-20 kabla haijapotelea hewani.

Tabaka la pili ni ile harufu inayotokea mara baada ya ile ya kwanza kupota. Hizi zinakaa kati ya saa 3-6 kwenye ngozi baada ya kujipulizia pafyumu.

Tabaka la mwisho ni harufu nzito na kubwa na inapotelea hewani kwa polepole sana.. Ni hili linaipa pafyumu nguvu ya mwisho. Baada ya kupuliza pafyumu tabaka hili utalisikia kuanzia nusu saa hadi saa nzima. Harufu yake inanukia hadi masaa 24 mwilini.

Pafyumu zipo za aina mbalimbali. Zile zenye harufu ya maua ni nyingi na zinamfaa kila mtu na walau kwa kila tukio. Pafyumu hizi zina harufu za maua kama rozi, jasmine na malili. Pafyumu zenye harufu za miti/misitu zina harufu nzito na nyingi ni za kiume kwa mfano pafyumu maarufu za Elizabeth Arden. Zile zilizotengenezwa kwa kutumia viumbe wa baharini nyingi ni za vijana. Pafyumu zilizotengezwa kwa viungo na matunda kama vile matunda ya ndimu, zabibu, chungwa na matikiti maji zina harufu nyepesi kama vile pafyumu za Dior Addict 2.

Kuchagu pafyumu sahihi inaweza isiwe rahisi kwako ila kwa dondoo chache utafanikiwa. Pengine hutakuwa na muda wa kujaribu pafyumu zote ila unachoweza kufanya ni kujaribu moja kila ukiwa kwa muuzaji. Pulizia kidogo kaganjani na fuatilia siku nzima jinsi inavyonukia, vyema ukumbuke zile tabaka tatu .Pia usijaribu ndani ya duka la muuzaji na kufanya uamuzi wa kununua kwa kuwa kutakuwa na harufu za pafyumu mbalimbali hivyo hutaweza kujua harufu halisi ya unayotaka kununua. Je harufu yake inaisha kabisa baada ya dakika kumi tuu au imenukia hadi ukaona inakuzidi nguvu? Kitu kimoja ukumbuke ni kuwa usiwe umevaa pafyumu nyingine tayari kwani  harufu zitakuchanganya.

Maduka mengi makubwa ya pafyumu yana wasaidizi wanaojua kazi zao kwa hiyo ukiwaambia ni pafyumu gani hasa unatafuta kwa mfano harufu upendayo au mahali na wakati utakapoitumia watakuwa tayari kukuelekeza. Pafyumu za kuvaa mchana ni za harufu ya matunda na zile za jioni ni za harufu nzito kama vanila. Pia binadamu wamejiwekea viwango kutofautisha pafyumu za kike na za kiume. Kama maandishi hayajasema kama pafyum husika ni ya kike au kiume watu wamepitisha kuwa pafyumu zenye harufu nyepesi, za sukari, matunda na maua ni za kike. Zile zenye harugu nzito ni za kiume, ni kama vile ngumu kuelezea.

Sasa wakati wa kuchagua pafyumu zingatia yafuatayo:
Mahali: Ni wazo zuri kufukiria ni wapi unaenda wakati unataka kutumia pafyum husika. Kwa mfano kama unavaa kwenda kazini tumia pafyumu ambayo ni safi na nyepesi. Harufu nzito zinaweza kukuzidi kwenye kichumba kidogo cha ofisi na pia wenzio wanaokuzunguka wanaweza kukereka na harufu ya pafyumu yako. Pafyumu zenye harufu za matunda na maua ni chaguzi nzuri kwa kazini, shuleni ama maeneo ambayo hayako wazi wakati zile nzito zinafaa kwenye sherehe za nje na matukio rasmi ya jioni. Chagua pafyumu wakati wa mchana kwa kuwa seli za mwili zinazotambua harufu ndio zinafanya kazi vizuri zaidi.

Majira: Kuna aina za pafyumu ambazo ni maalum kwa majira fulani ya mwaka. Badili pafyumu kuendana na majira. Pafyumu zenye harufu kali na ya viungo zinaweza kukera wakati wa kiangazi ila zikafaa sana wakati wa masika. Pafyumu zenye harufu za maua ni nzuri sana kwa kipupwe wakati zile nyepesi zenye harufu ya utamu na matunda zinafaa zaidi wakati wa miezi ya kiangazi. Pafyum zenye harufu za vyakula kama vile vanila na kitunguu saumu ni sahihi kwa majira ya baridi. Pia kutumia pafyumu ambao itakukumbusha matukio muhimu kama siku yako ya harusi au likizo eneo fulani la dunia ni njia nzuri kujipa kumbukumbu nzuri siku nzima

Kama ngozi yako ni kavu unahitajika kutumia pafyumu zaidi ya mwenye ngozi ya mafuta. Tumia pafyum baada ya kuoga na kujikausha kabisa. Usichanganye pafyumu na deodorant au sabuni ya deodorant kwa kuwa harufu zitagongana na kufanya harufu mbaya.

Makala hii imeandaliwa na Vivi O. Machange 0755 2000 23 

No comments:

Post a Comment