Pages

Friday, September 20, 2013

friday finest

marafiki zangu wa kweli watu wangu wadogo leo nimewatembelea uani. sakafu ya uani kwao ni ya c-tiles. vi tile hivi ni vizuri kwani vinafanya uani kuwe nadhifu na huwa havina utelezi iwe ni wakati wa mvua au hata wakati wa kuvisafisha. vimifereji wa c-tiles ni vigumu kufagia bila maji kwani michanga haitaondoka kwahivyo kwa kusafisha sakafu ya c-tile itakate vizuri inabidi ufagie kwa fagio na maji. c-tiles zinapatikana kiwandani wanakotengeneza kule chang'ombe, ziko za rangi ya mvi, nyeupe na nyekundu. unaweza kuweka za rangi moja ama kuchanganya rangi kama hapa kwa watu wangu wadogo. ukiviweka uani kwako hutakaa ujutie uamuzia wako!
kwenye floor hii c-tiles zimechanganywa nyekundu na nyeupe

mvua ikinyesha c-tiles zinachukua dk 1 kukauka hasa kama fundi aliweka slope nzuri

hakuna tope kukiwa na c-tile

mambo yote uani ni kwa floor ya c-tile

No comments:

Post a Comment