Pages

Wednesday, September 18, 2013

nyumba ni mawe

sio siri ninapenda makazi mazuri yenye kazi za mawe na huwa nikiyaona nayachungaza kwa undani na kutafakari kwa kina. ninafurahia kuona vitu vimejengwa vizuri kwani huwa naamini mwenye hiyo nyumba anakuwa amefanikiwa kuifanya ndoto yake kuwa kweli kwa kuweza kupata mafundi waliomfanyia kazi ambayo hata mimi mpita njia nikiiona naifurahia. leo nimeamua ku blog kazi za mawe ambazo zinaifanya nyumba iwe sehemu imara.
mawe ya kukanyagia ambayo yanasaidia kuunganisha bustani na sehemu nyingine za nyumba
vitofali vya chini (paving blocks) ambavyo fundi anaweza kukutengenezea kwa umbo unalotaka na pia unaweza kuweka rangi kama kijani au nyekundu
ukuta uliowekwa mawe ya Tanga ambayo yaweza kuwekwa hata sakafuni pia

mawe ya sakafuni ambayo yametenganishwa kwa changarawe.buni kadri uwezavyo, wanasema sky is the limit

ukuta mfupi wa mawe. wafaa hasa kwa wale wenye makazi ya karibia na bahari


haya yamewekwa ili kutengeneza njia ya miguu

No comments:

Post a Comment