Pages

Thursday, January 8, 2015

habari ya mtambo wa kubadilisha maji kutoka kwenye chumvi kwenda yasiyo na chumvi ni njema kuliko!

Yani nilipoona habari hii nimetamani kama wangezindua pia vimtambo vidogo kwa ajili ya majumbani. Watu wengi wengi hawana uhakika wa maji safi na salama, na huwa naamini suluhisho kamili na la kudumu ni kuchimba kisima, ila tatizo sasa linakuja kuwa asilimia kubwa ya maji ya visima ni ya chumvi. Sasa  hili la kuweza kuwa na mtambo wa kuyabadilisha toka kwenye chumvi kwenda yasiyo na chumvi (safi na salama) ni njema sana kwakweli. Process ya kubadili maji ya chumvi kwenda yasiyo na chumvi inaitwa desalination.
soma hapa:
Naibu Waziri wa Miundo mbinu na Mawasiliano Issa Haji Ussi (Gavu)akitoa hotuba wakati alipofungua mtambo wa kubadilishia maji kutoka kwenye chumvi na kuwa safi na salama Uzi Ng'ambwa Wilaya ya kati Unguja ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 51ya Mapinduzi ya Zanzibar.kulia yake nimuakilishi wa Taasisi ya Mork Water Solution ya Ujarumani Mikalen na kushoto yake ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Idriss Muhsin Hijja.
 Wananchi mbalimbali wakinywa maji yaliobadilishwa kutoka kwenye chumvi na kuwa safi na salama baada ya kufunguliwa huko Uzi Ng'ambwa Wilaya ya kati Unguja ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 51ya Mapinduzi ya Zanzibar

No comments:

Post a Comment