Pages

Wednesday, February 25, 2015

H. Baba: Tunazaa kwa mipango na Flora

STAA wa Bongo Fleva, Hamis Ramadhan ‘H. Baba’, ni kama amejibu maneno yaliyokuwa yakizungumzwa na mashabiki wake juu ya ujauzito wa mkewe, baada ya kudai kuwa wanazaa kwa mipango.
H.Baba aliyasema hayo hivi karibuni na kusema kuwa yeye na mkewe ambaye pia ni mwigizaji wa filamu, Flora Mvungi, wamepanga kuzaa kulingana na mahitaji yao na muda wautakao, hivyo maneno yanayosemwa juu ya Flora kubeba mimba mtoto wao Tanzanite akiwa bado mdogo ni kuwakosea na kuingilia maisha yao.

Alisema wao ndio wanaojua familia yao itaishi katika mazingira gani, hivyo kila watakapohitaji mtoto watazaa kwa kuwa uwezekano wa kupatikana upo miongoni mwao.


“Ninaona sehemu tofauti watu wakizungumza juu ya ujauzito wa mama Tanzanite, amewahi kubeba mimba huku wakisahau kuzaa ni mipango ya mwanamke na mwanaume, alafu hakuna tutakayemuomba msaada kwa ajili ya familia yetu, hivyo tutazaa kila tunapoona muda umefika,” alisema.


Alisema ili kuhakikisha wapo makini katika suala la watoto wao, kila mmoja wanamuwekea mipango bora kwa ajili ya maisha yake na ndio maana yeye na mkewe wanatumia njia na mbinu nyingi kusaka fedha zitakazotunza vizazi vyao
.
Chanzo; Mtanzania

No comments:

Post a Comment