Pages

Sunday, February 22, 2015

JACK PENTEZEL awajia juu wafitini wa penzi lake

Akizungumza na Mwananchi Jack alisema kuwa hana tatizo katika ndoa yake lakini anasikia kwa watu wa karibu kuwa kuna madai yamezagaa yeye na Dibibi wana mgogoro mzito.
Mwigizaji Jack Pentezel amewajia juu wale wote wanaotaka umaarufu kupitia jina lake kwa kutangaza kila kukicha kuwa ameachana na mumewe Kauthar  Dibibi.

Alisema kama kuliwahi kutokea kutokuelewana na mumewe basi ni vitu vya kawaida lakini siyo mgogoro mkali kama watu wanavyovumisha, “Sina ugomvi na Dibibi na nimetoka kuzungumza nae muda siyo mrefu, huo ni uvumi na siku nyingi wamekuwa wakivumisha hivyo, kwa sababu wanatuona tunapendana, ”alisema Pentezel.

Mwishoni mwa mwaka jana kulikuwa na uvumi kuwa wawili hao wameachana kutokana na kuwa na ugomvi unaosababishwa na tabia ya mwanadada huyo kuzurura na mashoga na kusahau majukumu ya nyumbani kama mke.

“Hivi akinikataza kuwa na marafiki au niwahi kurudi, si atanikataza na kuigiza kabisa kwani kuna wakati tunafanya kazi hadi muda mbaya, ”alisema Jack.

Kwa upande wa mume wa mwigizaji huyo, alisema kuwa hawana tatizo na mkewe na akichelewa kurudi anamuuliza kawaida kama ambavyo hata yeye akichelewa atamuuliza na wala siyo kwa sababu ya marafiki.

“Nafahamu kazi ya mke wangu, analazimika muda mwingi kuwa na marafiki ambao anafanya nao kazi, simzuii ingawa siwezi kuruhusu azurure kama wanavyodai,  bali natoa ruhusa kwa safari zinazotambulika, ”alisema Dibibi.

Dibibi aliongeza kuwa kwa sababu wanapendana watasikia mengi  yanayowahusu ili kuwakatisha tamaa, lakini kwa sababu walijipanga tangu mwanzo hawalihofii hilo.

Mume wa mwigizaji huyo alieleza kuwa imekuwa kawaida kwao kusikia hili na ile na ikitokea kukawa na ugomvi wa kweli kati yao wapambe watafurahi maana baada ya kuwaombea mema wanawahesabia siku. Alifafanua kuwa hayo mambo ndiyo yanagharimu ndoa za wasanii wengi halafu jamii huwatizama kwa jicho baya kwenye suala zima la uhusiano.

“Kuna wanaowaona wasanii hawadumu kwenye ndoa, ni kweli ndoa nyingi zimevunjika, tangu nimuoe Jack naelewa sababu ya kuvunjia kwa ndoa hizo ni maneno kutoka kila kona, marafiki unaoamini ni wema wanajidai wanafahamu mabaya ya mkeo, wafitini nao mazungumzo ni hayo, nimejifunza kupuuza.


Alisema kuwa pamoja na kumuonea wivu hayapi nafasi maneno ya mtu yeyote na huamini ukweli anaosikia kutoka kwa mkewe na hufanyia kazi anachoamini kina mashaka na makosa kama wafanyavyo watu wengine.

No comments:

Post a Comment