Pages

Thursday, February 26, 2015

KUTOKA KWANGU: Jinsi unavyoweza kuipa sebule yako identity

Kama wewe ulivyo na kitambulisho na sebule yako vilevile yaweza kuwa na kitambulisho chako. 

Zifuatazo ni njia chache kwa ufupi sana unazoweza kukamilisha kitambulisho chako kwa sebule yako.

Weka vitu vya ladha yako, yaani vile unavyopenda wewe bila kufuata kanuni uliyosoma popote. Hii inaweza kuwa ni fremu za picha za familia au kama ni mpenda sanaa za ukutani basi tundika. Unaweza pia kutundika nukuu (quotes) unazozipenda. Nukuu hizi labda ulizisikia kwa mwalimu wako wa primary, au popote ziandike, zitengenezee fremu zitundike, kumbuka pia hata rangi ya hizo fremu inahusu utambulisho wako, labda unapenda orange, nyekundu nk.

Kama unasafiri sana sehemu mbalimbali za dunia, unaweza kujumuisha sebuleni kwako chochote toka nchi hizo ulichonunua ulipokuwa huko.

No comments:

Post a Comment