Pages

Wednesday, February 11, 2015

KUTOKA KWANGU: Aina mbalimbali za viti vya nyumbani kwa matumizi tofauti tofauti

Kuna aina nyingi nyingi za viti na hapa ni baadhi. Kuna kiti cha ku fit kila hitaji na kila eneo kwahivyo ni vyema kutafiti aina zote zilizopo kabla hujaamua. Hapa sitazungumzia viti vya meza ya dining kwa ajili ni seti moja na meza yake.
Kiti hiki kwa wengi kinajulikana kama kiti cha mabawa, kwasababu ya hii feature iliyoko ubavuni ambayo inasevu kama kizuizi iwe ni sehemu jua linapiga kwa ubavuni kwa mfano. Kwa wale watu wazima/wazee wanaosinzia kwenye kiti mchana mabawa ya kiti hiki yanasapoti kichwa.


Hivi hapa viwili ni viti kwa ajili ya kujinyoosha moja kwa moja bila kuweka miguu kwenye kitu kingine cha kuisapoti. Mgongo unajikunja kidogo na kwa ajili kiti hiki ni kwa ajili ya burudani zaidi mara nyingi unakikuta kimewekwa kwenye varanda au eneo lingine nje ya nyumba. 

Hiki kiti kinafaa kwa kila tukio, na ndio kilivyo. Ni kiti cha ziada kinachotumika pale unapokuwa na ugeni mwingi sebuleni. Sebule nyingi kunakuwepo na kiti hiki (kwa kawaida wenyeji wanapendelea kuweka viwili) kutokana na muonekano wake unaovutia zaidi ya lengo lenyewe.
Mikunjo ya kiti hiki imekipa umaarufu toka historia ya fenicha, kimekaa kisanaa zaidi.
Hili sio sofa bali ni kiti kama tutakubaliana kuwa kiti ni kwa ajili ya mtu mmoja tu, kiti hiki kinaitwa kiti na nusu kwa ajili ni kupana kidogo zaidi ya kiti na ni kidogo kuliko sofa la mapenzi. Kiti na nusu kina matumizi mengi na unaweza kukikuta ndani ya nyumba kama vile kwenye sebule ndogo na chumba cha kulala. Tukutane kwenye post nyingine ya kutoka kwangu....utapenda

No comments:

Post a Comment