Pages

Thursday, February 12, 2015

KUTOKA KWANGU: Jinsi ya kutupia mito ya mapambo kwenye sofa zako



Mito ipo mingi na kwa bei nafuu na wadada/wamama tunainunua na kuitamani. Tatizo linakuja je, ni kwa vipi tunaitupia kwenye makochi yetu? Ununue ya size gani na mingapi na rangi zipi, inaweka kukupa changamoto kwakweli.
Na pia fahamu kuwa kubadilisha mito kila kipindi ni njia nzuri ya kuhuisha sebule yako bila kutumia gharama kubwa. Kwahivyo kufahamu ni kwa vipi uitupie ni skill eti. Hapa nakupa njia 2 za kutupia mito yako. Njia ya kwanza ni kama hiyo hapo juu ya kutupia mito ya ukubwa sawa upande wa kulia na kushoto(ikiwa inatazamana) halafu kati unatupia wa umbo tofauti. Hakikisha kochi lako lote hakuna sehemu iliyobaki loose.




Njia ya pili ni hii ya kuwa na seti mbili za mito ya size na umbo sawa lakini rangi tofauti huku ukutupia mito yote mstari mmoja ikilaliana mmoja juu ya mwingine kama picha hapo juu zinavyoonekana.













No comments:

Post a Comment