Pages

Saturday, February 7, 2015

KUTOKA KWANGU: Mitindo mbalimbali ya milango ya mbele ya nyumba

Mlango wa mbele wa nyumba unakuwa katikati ya nyumba na ndio unaowakilisha mvuto wa nyumba kwa hivyo muhimu uwe maridadi. Wengine wanapendelea kuweka glass panels kwenye mlango wa mbele kama hivi kwa ajli ya kuongeza mvuto na mwanga ndani.
Swala la security kwa hapo kwenye glass sio issue kwa ajili kwa ndani kunakuwa na chuma, na wengi wetu tunaweka mlango wa mbao pamoja na grill.

Milango hii ipo ya malighafi na designs nyingi mno wewe tu ushindwe, ipo ya chuma ambayo ikiwa imepakwa rangi kabla hujaigusa huwezi kutofautisha na mbao. Hii ya hivi inauzwa imeshatengenezwa na huwa kwa wale ambao kwa security wanaweka milango ya mbele miwili pamoja (wa chuma na wa mbao) endapo utaweka hii ya chuma huna haja ya kuweka tena wa mbao wala grill.

Mlango wa mbele huwa ni mpana kuliko milango mingine kwa kuwa upana wake ni sawa na upana wa corridor uliopo.

 Designs mbalimbali za milango ya mbele, hii imezibwa kote kote haina glass panels
Angalia glass panels za huu zilivyokuwa na shape moja na handle zake, unavutia

No comments:

Post a Comment