Pages

Wednesday, February 25, 2015

Stara Thomas akana kufumaniwa na mpenzi wake

Aliyekuwa mwimbaji muziki wa gospel na baadaye kurudi kwenye bongo fleva Stara Thomas, amekana habari zilizoenea hivi karibuni kuwa amefumaniwa na mpenzi wake nyumbani kwake.

Akizungumza na Soudy Brown kupitia Uheard alisema kuwa mwanamke kama yeye hawezi kufumaniwa na kwamba mpenzi wake wa sasa kinachomsumbua ni wivu wa kimapenzi bila kumtaja jina mpenzi wake huyo wa sasa.

Aidha ameongeza kuwa hayuko tayari kuzungumzia swala hilo kwa sasa ndio maana amekaa kimya tangu habari hizo zitoke kwenye magazeti.
"Nimeamua kunyamaza kimya lakini ipo siku ntazungumza kila kitu kuhusiana na habari hizi," alisema Stara.

No comments:

Post a Comment