Pages

Saturday, February 14, 2015

Wahenga walisema pombe si chai...

MWANAMKE mmoja mkazi wa Kijiji cha Italala, Kata ya Sepuka Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Mwamvua Alli anadaiwa kumvunja mume wake mguu wa kulia na kumshambulia kwa kitu kizito kichwani.
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni majira ya saa 1:30 usiku ambapo wote walikuwa wamelewa na kumsababishia maumivu makali.

Akizungumza na majira Mwenyekiti wa kijiji hicho, Shabani Makonga Guda (SMG) alisema mwanamke huyo alimpiga mumewe Selemani SangÆwa (66) na kumuumiza vibaya katika ugomvi uliotokea kati yao wakiwa wamelewa ambapo mume wake alidai mkewe alichelewa kurudi nyumbani.

Habari zinasema katika ugomvi huo Selemani alimpiga mke wake kwa fimbo ya nguvu baada ya mabishano, mke akapata maumivu makali na hiyo ni kwa sababu Mwamvua alitoa majibu mabaya yaliyomfanya Selemani akasirike, mke kuona hivyo akampiga mume wake 'ngwara' akaanguka chini na wakati yuko chini alichukua mti uliokuwa karibu akampiga mumewe mguuni, kichwani na kifuani na kumuumiza vibaya.

Makonga alipigiwa simu juu ya tukio hilo kutokea kwenye nyumba ya Selemani na alipofika akaagiza gari na lilipofika likawachukua wote hadi Kituo cha Polisi Sepuka kupata hati ya matibabu.


Aidha, alikimbizwa Hospitali ya Misheni Puma na hadi sasa bado anatibiwa mguu bado unauma na jicho bado haliko kwenye hali nzuri, aidha mke wake amewekwa rumande Singida akingojea hatua zingine za kisheria zifuatwe.

No comments:

Post a Comment