Pages

Thursday, February 26, 2015

Wanaume watatu waoana Thailand

Wanaume watatu waliofunga ndoa siku ya wapendanao (Valentine) nchini Thailand wamepata umaarufu katika mtandao baada ya picha za maandalizi ya harusi hiyo kuenea mitandaoni.

Watu hao walijulikana kama Joke,Bell na Art ambao walioana saa sita, usiku wa tarehe 15 mwezi Februari mwaka huu.

Kulingana na gazeti picha hizo zinawaonyesha wanandoa hao watatu wakiwa wamevalia nguo za utamaduni wa Thai uliochanganyika na utamaduni wa magharibi.

Ujumbe mmoja ulioandikwa katika katika picha moja ulisoma' mapenzi ya kweli hayawezi kuonekana na macho pekee'.

''Iwapo unataka kujua thamani yako basi ni lazima uione na moyo wako''.
katika mtandao wa facebook wa runinga moja ,picha ya wanandoa hao ilipendwa na zaidi ya watu 50,000 huku watu 1000 wakitoa maoni yao.
Chanzo BBC 

No comments:

Post a Comment