Pages

Friday, February 13, 2015

Waziri Nyalandu: Mimba ya Aunty Ezekiel si yangu

Waziri wa maliasili na utalii Mh. Lazaro Nyalandu amefunguka kuhusiana na taarifa zilizoenea kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na muigizaji wa filamu za Kibongo,Aunty Ezekiel na kwamba ujauzito alionao msanii huyo ni wa kwake.
Mh.Nyalandu amekanusha habari hizo kupitia kupindi cha leo tena cha Clouds Fm wakati alipokuwa akihojiwa na mtangazaji wa kipindi hicho Husna Abdul ambapo pia alikuwa ameambatana na mkewe Faraja Kota. 

Aidha alisema kuwa habari hizo zilitolewa na gazeti moja la hapa nchini kuwa waziri huyo alitumia mamilioni ya pesa za umma kuponda raha na msanii huyo,wakati huo alikuwa nchini Marekani kikazi kwa mwaliko wa ubalozi wa nchini humo ambapo wasanii wawili wa hapa nchini Aunty Ezekiel na Kassim Mganga nao walikuwa wamealikwa.


‘’Kwa mara ya kwanza nilimuona msanii huyo kwenye mwaliko huo na baada ya hapo nikaondoka zangu sikuonana naye tena hata namba yake sina hapo ndipo habari zikaenea kuwa nimetembea naye mara mimba aliyonayo ni yangu kwa kweli nilishangaa sana,’’alisema Nyalandu. 

‘’Naamini taarifa hizo zilizidi kuzungumzwa zaidi na maadui zangu wa kisiasa baada ya mimi kutangaza nia ya kugombea urais uchaguzi mkuu ujao,’’alisema Nyalandu.

Hata hivyo Faraja akizungumzia kuhusiana na taarifa hizo alisema kuwa hazikumshtua hata kidogo kwa maneno kuhusu mumewe amekuwa akiyasikia sana na ameshayazoea na anampenda sana mumewe.

(By the way Faraja amependeza na kilemba chake)

No comments:

Post a Comment