Pages

Sunday, February 22, 2015

WIVU WA MAPENZI: Mke amkata mume sehemu za siri

Oh my Oh my..kuna vituko, alimvizia akiwa amelala ama??
Chanzo ni ugomvi unaohusishwa na wivu wa mapenzi.
Songea. Mkazi wa Kijiji cha Majimaji, Kata ya Chalinze, wilayani Tunduru (jina linahifadhiwa), anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumkata sehemu za siri mume wake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msikhela alisema kuwa tukio hilo limetokea jana saa tisa usiku baada ya kutokea mzozo kati yao.

Kamanda Msikhela alisema mwanaume huyo (jina linahifadhiwa), amejeruhiwa sehemu za siri na kwamba chanzo cha yote hayo ni wivu wa mapenzi.

Alisema majeruhi huyo kwa sasa amelazwa Hospitali ya Wilaya ya Tunduru na hali yake inaendelea vizuri.

“Tunamhoji mtuhumiwa ili kujua sababu, tukikamilisha uchunguzi tutamfikisha mahakamani kujibu mashtaka,” alisema Kamanda Msikhela. 
Chanzo Mwananchi

No comments:

Post a Comment