Pages

Saturday, March 14, 2015

HEBU TUPELELEZE NYUMBA....UNAZINGATIA NINI UNAPOTAKA KUNUNUA FIMBO ZA PAZIA..

Kama hauna uzoefu nazo unapotaka kununua fimbo za pazia unaweza kudanganyika na muonekano. Kwangu mimi nashauri kitu muhimu cha kuzingatia sio muonekano bali ni
unene wa ile sehemu fimbo inaposhikana na ukuta. 
Fimbo hii ni sahihi zaidi kwani hata pazia zikivutwa chini na watoto watundu fimbo haivunjiki kwakuwa kishikizo cha ukutani ni kinene.
Fimbo hii japo ni ya chuma lakini sishauri kwani sehemu ya kushikana na ukuta ni nyembamba kiasi kwamba ni rahisi ku bend kama hii pacha hapa chini.
Hapa fimbo kishikizo cha fimbo ukutani kimejikunja, na ukitaka kukirudishia juu vizuri kitaishia kuvunjika.

No comments:

Post a Comment