Pages

Thursday, March 12, 2015

HII NI KWA WALE WENYE CHUMBA KIMOJA....UNAVYOWEZA KUWEKA MPANGILIO ILI KISIONEKANE KAMA STOO

Hakuna ubaya wa kuishi kwenye chumba kimoja kama uko mwenyewe na ndio unaanza kujitegemea, ila ili kisionekane kurundikana fanya vitu viwili ambavyo binafsi naviona ni muhimu sana. Vitu hivyo ni
kuongeza eneo la kuhifadhia na kuwa na vile vitu unavyohitaji/unavyotumia kwa wakati huo tu.

Kwa kuongeza sehemu ya kuhifadhia unaweza kutengeneza sofa, kitanda na meza zenye sehemu ya kuhifadhia mvunguni, ambapo maeneo haya unaweza kuhifandhi vitu vingi sana, hata viatu ukitoka kazini unamwambia mtu anakufutia vizuri halafu unahifadhi kwenye droo ulizotengeneza chini ya chaga. 

Milango ya ndani ya kabati la nguo iwe na kulabu (hooks) kwa ajili ya kutundikia chochote cha kufaa kutundikwa kama vile mikoba, mikufu nk.

Kwa upande wa kuwa na vitu unavyotumia kwa wakati huo tu ni kwa mfano, tengeneza sofa moja ya siti 3 au mbili na sio zaidi kwani kwa chumba kimoja huhitaji zaidi, huna haja ya kuwa na nguo, viatu, vyombo ambavyo hutumii kwa wakati huo.

Hope wadada/wakaka wenye chumba kimoja somo limeeleweka. Hapana ishi stoo..

No comments:

Post a Comment