Pages

Thursday, March 5, 2015

KUTOKA KWANGU: Unajua kama unaweza kufremu mwenyewe picha zako na za familia yako?

Huenda unajisikia kama kufremu mwenyewe picha zako ni kazi kubwa mno kwako. Ni rahisi mno pale unapokuwa na fremu tupu, picha, mkasi, tape na glue. Fikiria jinsi ulivyokuwa na picha za digital nyingi! Picha hizo zote za familia ulizopiga ambazo hujaweza kufremu hata, sana sana umepeleka kwa wasanii kufremu mbili au tatu tu. 

Picha za kufremu mwenyewe zinaweza kuwa zawadi kwa mwanafamilia pale kunapokuwa na tukio labda ni siku ya kuzaliwa kama ni mwanao unamfremia picha zake kadhaa ndani ya fremu moja toka utotoni hadi hapo alipo na ndipo unampa hiyo fremu kama zawadi.

Ukiweza kuwa na muda wa kufremu picha zako mwenyewe unakuwa na suluhisho lako mwenyewe ambalo litafanya kazi kuendana na matakwa na muda wako!

No comments:

Post a Comment