Pages

Tuesday, March 3, 2015

Mchezaji wa Sunderland akamatwa na polisi kwa tuhuma za kufanya mapenzi na binti mwenye miaka 15


                       
 Adam Johnson mchezaji wa Sunderland ya England
Mchezaji wa timu ya taifa ya England ambaye pia anakipiga katika klabu ya soka Sunderland Adam Johnson amekamatwa na polisi kwa tuhuma za kufanya mapenzi na msichana mwenye umri wa miaka 15.
Polisi katika eneo la Durham wamesema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 amekamatwa mapema wiki hii kwa tuhuma za kufanya ngono na binti mwenye umri wa chini ya miaka 16, na amebaki chini ya ulinzi. Taarifa ndani ya klabu yake zinasema kuwa mchezaji huyo amesimamishwa kusubiri matokeo ya uchunguzi wa polisi.

Taarifa za kukamatwa kwake zilitolewa mapema kupitia gazeti la The Sun. Kukamatwa kwake kunakuja muda mfupi kabla hajasafiri na timu yake ya Sunderland kwenda kukutana na Hull kwa michezo ya Ligi kuu ya England iliyopangwa kuchezwa leo usiku. Sunderland imesema haitaendelea kuzungumzia kukamatwa kwa mchezaji wake.

No comments:

Post a Comment