Pages

Monday, March 9, 2015

MWANAMUZIKI SARAHA AFUNGUKA KUHUSU UHUSIANO WAKE NA FUNDI SAMWELI

Fundi Samweli na Saraha enzi za penzi lao
Staa wa muziki Saraha, amefunguka kwa mara ya kwanza kabisa tangu kuvunjika kwa mahusiano yake na mtayarishaji muziki maarufu Fundi Samweli'
kupitia mahojiano yake na eNewz ameeleza kuwa mapenzi sio suala rahisi
na kusisitiza kuwa hakuna shida yoyote kubwa iliyosababisha kutengana kwao.

Saraha ameieleza eNewz kuwa, safari yao ya mahusiano ilifikia mahali ambapo kila mmoja aliona kuna umuhimu wa kuchukua njia yake tofauti, huku akisisitiza kuwa kwa sasa, mpenzi wake mkubwa ni muziki tu ambao yupo nao wakati wote.

Saraha amesema kuwa, anajipanga kwa ajili ya kurejea nchini ndani ya miezi kadhaa kwa ajili ya upigaji picha za video yake mpya katika kuthibitishia mashabiki kuwa muziki, hususan ule wa Bongo Flava ndio mpenzi wake mkubwa sasa.


No comments:

Post a Comment