Pages

Tuesday, March 17, 2015

NEY WA MITEGO HATAKI MWANAMKE....

Ikiwa imepita miezi isiyopungua mitano baada ya msanii Ney wa Mitego kumpata mwanae wa tatu anayefahamika kwa jina Curtis, staa huyo ametoa kauli nzito kuwa kwa sasa hana mahusiano wala mapenzi yoyote kwa wamama wa watoto wake.

Kauli hiyo iliyoonekana kuwashangaza mashabiki wa msanii ambapo Ney pia amesema kuwa mapenzi  
yake yote kwa sasa yapo kwa wanawe tu.

Ney ambaye kwa sasa pia kuna tetesi za kuwa anatarajia mtoto mwingine, tetesi ambazo amezikanusha kiutata, amesema kuwa kwa sasa hahitaji kabisa mwanamke, na watoto wake pekee ndio wanampa nguvu na kumhamasisha kujituma kila siku.
Chanzo: EATV

No comments:

Post a Comment