Pages

Sunday, March 15, 2015

UUME WA KUPANDIKIZA WAFANIKIWA AFRIKA KUSINI

Kundi la madaktari wa upasuaji kutoka Afrika kusini limefanikiwa upandikizaji wa uume wa mwanadamu.

Oparesheni hiyo iliochukua masaa manane ilifanywa mnamo mwezi Disemba katika hospitali ya Tygerberg mjini Cape Town kupitia ushirikiano wa chuo kikuu cha Stellenbosch.

Inadaiwa kuwa ni jaribio la pili la upasuaji huo kufanywa.
Madaktari wanasema kuwa mgonjwa aliyefanyiwa upandikishaji huo amepona.

Uume wake ulikatwa baada ya matatizo yaliosababishwa na kupashwa tohara.
Chanzo: Daily Sun

No comments:

Post a Comment