Pages

Thursday, March 5, 2015

Wajawazito watakiwa kwenda kliniki na waume zao. Wapo wanaoenda peke yao na kujitetea kuwa wanaozaa nao ni waume za watu!

Haluuu, hivi kama wewe muuguzi mjamzito akishakuambia kuwa ninayezaa naye ni mume wa mtu, utafanyaje? Itabidi umsaidie tu..

Wajawazito nchini wametakiwa kuwashirikisha waume zao kliniki kwa kupewa huduma na vipimo mbalimbali kwa ajili ya ukuaji wa mimba hadi watakapojifungua.
Hayo aliyasema Mkurugenzi wa asasi ya kiraia ya Tupawaki inayoundwa na Umoja wa Wanawake Kihonda, Mariam Makulo kwa ushirikiano na wakazi wa Vijiji vya Chakwale na Iyogwe wilayani Gairo katika kongamano la ufuatiliaji matumizi ya mafungu ya fedha na utoaji huduma za afya vijijini.

Makulo alisema wanawake wengi wajawazito wa mjini na vijijini wamekuwa wakitoa visingizio pindi wanapotakiwa kuongozana na wenza wao katika vituo vya afya.

Alisema wanawake hao wamekuwa wakidai kuwa, wanaume waliozaa nao ni waume za watu bila kujua wanawapa mauguzi wakati mgumu ikiwamo kushindwa kutekeleza malengo ya utoaji wa elimu ya uzazi salama katika ngazi ya familia.

Makulo alisema mafunzo hayo ambayo yamekuwa yakifanywa katika vijiji mbalimbali wilayani Gairo yamefadhiliwa na mfuko wa The Foundation for Civil Socity kwa lengo la kuelimisha jamii kuhusiana na suala la ufuatiliaji wa afya ya uzazi.
Chanzo Mwananchi

No comments:

Post a Comment