Pages

Thursday, March 12, 2015

WANAFUNZI WA DARASA LA PILI NA LA KWANZA MOSHI WAKUTWA MIGOMBANI WAKILAWITIANA...HALAFU UNAJUA KILICHOFUATA NINI....MZAZI MMOJA AKAJA KUWAPIGA WALIMU KWA KUMDHALILISHA MWANAE

WANAFUNZI wawili wa darasa la pili katika Shule ya Msingi Ongoma iliyopo Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro wamekutwa wakilawitiana katika shamba la migomba jirani na shule hiyo.

Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo,
Jerad Kesi, aliiambia MTANZANIA jana kwamba tukio hilo lilitokea Machi
5 mwaka huu.


Kutokana na tukio hilo, Mwalimu Kesi alisema mmoja wa wazazi wa watoto hao alivamia shuleni hapo na kuwapiga walimu kwa kile alichosema kuwa walimu hao walikuwa wamemdhalilisha mtoto wake.

“Siku ya tukio, wanafunzi wawili wa darasa la pili na mmoja wa darasa la kwanza walikutwa na mwalimu wangu wakilawitiana kwenye migomba.
“Walipojua mwalimu amewaona, walikimbia na kuacha nguo zao pamoja na yule wa darasa la kwanza. Tulipomhoji yule mtoto aliyebaki alikubali kwamba amekuwa akilawitiwa na kwamba ameshafanyiwa kitendo hicho kama mara saba hivi,” alisema Mwalimu Kesi.

Baada ya wanafunzi hao kutimua mbio, Mwalimu Kesi alisema walirudi nyumbani na baadaye mmoja wa wazazi wao alifika shuleni hapo na kuwashutumu walimu hao kwamba wamemdhalilisha mtoto wake kwa kumvua nguo.

“Baada ya majibizano kati ya walimu na mzazi huyo, mzazi huyo aliwapiga walimu kwa fimbo na kuwajeruhi.
“Kwa hiyo, nilichokifanya nilikwenda kutoa taarifa polisi na kupewa RB namba MJ/RB/988/15 kwa ajili ya kumkamata mzazi huyo,” alisema mwalimu huyo.

Naye Mwalimu Idda Kilawe ambaye ndiye aliyewakuta
wanafunzi hao wakilawitiana, aliiambia MTANZANIA, kwamba siku ya tukio aliwakuta wanafunzi hao wakiwa ndani ya kibanda walichokuwa wamekijenga kwenye migomba.

“Niliwakuta wakiwa wamejenga kibanda cha miti na kukiezeka kwa matawi ya miti na ndani yake walikuwa wanafunzi watatu na wawili kati yao ndiyo walikuwa wakilawitiana.


“Nakumbuka siku hiyo nilikuwa natoka kuchukua matokeo ya mitihani na nilipokaribia eneo la tukio, nikasikia sauti za watoto. Niliposogelea eneo hilo niliwaona wanafunzi wawili wakiwa uchi na yule mdogo ndiye alikuwa amevaa sare. waliponisikia, wakakimbia,” alisema mwalimu Kilawe.

Mratibu wa Elimu, Kata ya Uru Kaskazini, Monyaichi Lyimo, alisema amekwisha kupata taarifa za tukio hilo.

No comments:

Post a Comment