Pages

Thursday, April 9, 2015

Ajali Iliyohusisha Magari Matatu Asubuhi Leo Eneo la Mkata Tanga Watu 10 Wamepoteza Maisha....Magari Hayo ni Basi la Ratco, Ngorika na Gari Dogo

Watu 10 wamefariki dunia katika ajali iliyohusisha magari matatu katika eneo la Mkata kijiji cha Mbweni wilayani Handeni Mkoani Tanga majira ya saa 5 asubuhi ya leo.

Akizungumza na East Africa Radio Kamanda wa
kikosi cha usalama barabara mkoa wa Tanga,  Mohammed Mpinga amesema kuwa ajali hiyo imehusisha mabasi mawili ya abiria na gari dogo katika barabara ya Dar es salaa kwenda Tanga na Arusha.

Kwa mujibu wa Kamanda gari dogo ilikuwa likitaka kulipita lori lililokuwa mbele yake na ndipo ilipogongana uso kwa uso na basi la Ratco lililokuwa likitokea Tanga kwenda Dar es salaam.

Baada ya basi la Ratco kugonganana na gari dogo, lilipoteza mwelekeo na kugongana tena uso kwa uso na basi la Ngorika lililokuwa likitokea Dar es salaam kwenda Arusha.


Aidha kamanda huyo amesema kuwa kati ya watu 10 waliofariki dunia ni wanaume watano wakiwemo dereva wa gari dogo na dereva wa basi la Ngorika pamoja na wanawake watano wakiwemo watoto wawili.

No comments:

Post a Comment