Pages

Monday, April 27, 2015

Aunt Ezekiel amewaambia wasanii waache kujipodoa kwenye msiba.....Wafanane na walioko kwenye majonzi

STAA wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel amewaponda wasanii wanaokwenda misibani wakiwa wamejipara kupita kiasi.

Msanii huyo aliwaponda wasanii wenzake wenye tabia ya kutumia sehemu za misiba kugeuza uwanja wa kuonyesha mavazi na vito vya thamani katika miili yao.

“Wenye tabia hizo acheni kujipodoa katika msiba, tunakera wenzetu ndiyo maana linaongelewa kila siku tuishi kulingana na utamaduni wetu tusiige,’’ alisema huku akifafanua zaidi.

“Wenzetu wakiwa katika majonzi nasi tufanane nao tusiende kuonyesha ujuaji wa kuvaa na kujipodoa kiasi cha kuwa kero kwa wanaotutazama,’’ alimaliza Aunt.

MTANZANIA

No comments:

Post a Comment