Pages

Saturday, April 25, 2015

Diamond amfagilia Zari kuwa anatimiza majukumu ya nyumbani.....Huku akimponda Wema kuwa hakufagia, kupika wala kufua nguo kulimshinda..

Diamond Platnumz, ambaye penzi lake kwa Zari limekuwa gumzo kubwa, ameweka bayana kuhusu kinachompeleka puta kwa msichana huyo wa Kiganda, akisema anachanganywa zaidi na rangi yake asili.

Wawili hao waliingia kwenye penzi zito
mwishoni mwa mwaka jana walipoanza kuonekana pamoja sehemu tofauti kabla ya kuweka bayana kuwa wana uhusiano wa kimapenzi.

Kabla ya hapo, penzi la Diamond na Wema Sepetu ndilo lililokuwa gumzo, lakini baadaye mwimbaji huyo wa kibao cha “My Number One” alieleza kuwa ameshafunga ukurasa na Miss Tanzania huyo wa zamani.

Akihojiwa hivi karibuni katika kituo kimoja cha runinga, Diamond alisema amekuwa akivutiwa kwa kiasi kikubwa na weupe wa Zari ambao hautokani na kipodozi chochote. “Zari ana vitu vingi, lakini binafsi nachanganyikiwa zaidi na rangi ndiyo ilivyo asili yake hakuna chochote anachotumia,” alieleza .

Diamond aliendelea kumwagia sifa mrembo huyo wa Uganda kuwa ni mwanamke anayeweza kutimiza majukumu yake kwenye nyumba licha ya urembo wake.

“Anafagia, anapika... kifupi kwake nimefika na hata familia yetu inamkubali, kwahiyo tafadhali watu waniache na mpenzi wangu,” alisisitiza

Diamond aliweka wazi kuwa alichelewa kumpata Zari na kumng’ang’ania Wema.

aliyekuwa mpenzi wake wa awali, Wema Sepetu kwa kuwa msanii huyo ambaye pia amewahi kutwaa taji la miss Tanzania alikuwa ni mtu wa kuendekeza starehe na hajui majukumu yake ya ndani kama mwanamke.

“Miaka yote niliyokaa na Wema, alikuwa hapiki, hafagia, hata kufua nguo zake tu zilikuwa zinamshinda na wakati wote mama yangu ndio alikuwa akitufulia.”alisisitiza mwanamuziki huyo.

MWANANCHI

No comments:

Post a Comment