Pages

Friday, April 10, 2015

Hofu ya Ugaidi SAUT yawafanya wanafunzi na mhadhiri kukimbia kimbia hovyo..


officialjestinageorgeblogPichani ni wanafunzi wa SAUT Mwanza wakiwa katika hali ya taharuki baada mwanafunzi mwenye asili ya kisomali (mwenye shati jekundu) kuingia kwenye darasa tofauti na analosoma kiasi cha kuwatia hofu kuu wanafunzi wa darasa hilo. 
Mashuhuda wanadai kuwa jamaa huyo alisimama mlangoni hapo na kumfanya lecturer aliyekuwa darasani kumfuata na kimuuliza yeye ni nani! Jamaa huyo hakujibu kitu licha ya kuulizwa mara tatu.

Baadaye aliondoka kimya kimya na kurejea tena akiwa na begi. Lecturer alimuuliza tena lakini hakujibu na kuanza kufungua begi lake. Kuona hivyo wanafunzi walianza kukimbia hivyo pamoja na mwalimu wao wakidhani ni gaidi. Mashuhuda wanadai wengi wameumia na kupoteza vitu hususan simu!
Kama ulikuwepo kwenye tukio naomba utujuze nini hasa kilitokea. 
Nimeskiliza voicenote aisee nimesikitika but nilicheka pale aliposema mwalimu nae katoka nduki lol!!! Haya jamani tuweni makini na tuendelee kumuomba Mungu ili amani iendelee kutawala nchi yetu. Washindwe na walegee wenye mipango na mawazo ya kuiletea shida taifa letu.#JestinaGeorgeBlog #DiasporaBlogger

No comments:

Post a Comment