Pages

Tuesday, April 21, 2015

HUZUNI.....MWANAFUNZI WA DARASA LA NNE SHULE YA MSINGI PUGU, FESTO FILBERT AKUTWA AMEJINYONGA CHUMBANI KWAKE.....HAKUACHA UJUMBE WOWOTE

MWANAFUNZI wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Pugu jijini Dar es Salaam, Festo Filbert (11) amekutwa chumbani kwake akiwa amejinyonga hadi kufa kwa kutumia mkanda wa kuvalia nguo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Mary Nzuki alisema tukio hilo lilitokea jana katika eneo la Majohe kwa Ngozoma.

Alisema sababu za kujinyonga mwanafunzi huyo bado hazijafahamika kwani hakuacha ujumbe wowote.

“Mtoto huyu alikutwa chumbani kwake anakolala akiwa peke yake, hakuna aliyejua sababu za kifo chake,” alisema.

Alisema maiti ya mwanafunzi huyo, imehifadhiwa Hospitali ya Amana na polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

MTANZANIA

No comments:

Post a Comment