Pages

Saturday, April 11, 2015

Jaji aagiza Justin Bieber akamatwe kwa tuhuma za kuwatuma walinzi wake wamshambulie mpiga picha

Jaji mmoja nchini Argentina ametoa agizo la kukamatwa kwa mwanamuziki Justin Bieber siku ya ijumaa akisema kuwa mwimbaji huyo alikataa kufika mbele yake kuhusiana na madai kwamba aliwaagiza walinzi wake kumshambulia mpiga picha mmoja mwaka 2013.

Jaji Alberto Julio Banos aliagiza kukamatwa kwa Bieber na walinzi wake Hugo Alcides Hesny na Terrence Reche Smalls.

Ujumbe uliotumwa kwa Bieber haukujibiwa mara moja.

Bieber anashtumiwa kwa kuwatuma walinzi hao kumshambulia mpiga picha Diego Pesoa nje ya kilabu moja ya Bueno Aires.

Msanii huyo hatahivyo hakurudi nchini Argentina ili kujibu maswali kuhusu kisa hicho.

Chini ya sheria za Argentina Bieber atakabiliwa na kifungo cha kuanzia mwezi mmoja hadi miaka sita jela iwapo atapatikana na hatia ya shtaka la kumjeruhi mpiga picha huyo.

BBC

No comments:

Post a Comment