Pages

Friday, April 17, 2015

Kajala Kutoka na Pishu Mei Mosi

MWIGIZAJI wa filamu nchini, Kajala Masanja ‘Kajala’ yupo katika hatua za mwisho kutoka na filamu yake mpya aliyoiita ‘Pishu’.

Filamu hiyo inatarajiwa kutoka siku ya wafanyakazi (Mei mosi) mwaka huu, ambapo katika filamu hiyo wasanii mbalimbali, akiwemo Hemedi Suleiman ‘PHD’, Mzee Onyango na wengineo wengi watakuwepo.

“Filamu hiyo ina mafunzo pamoja na kuchekesha, ni filamu itakayokuwa tofauti na nyingine kwa kuwa imeandaliwa katika ubora wa hali ya juu,’’ alisema Kajala.
MTANZANIA

No comments:

Post a Comment