Pages

Thursday, April 23, 2015

Mengi kutoa Milioni 50 kwa atakayefanikisha kukamatwa kwa waliowaua wafanyakazi wa kampuni ya Bonite Bottlers Moshi.

Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dakta REGINALD MENGI ametangaza zawadi ya Shilingi Milioni 50  atakayetoa taarifa itakayowezesha kukamatwa,kushitakiwa,watu waliowaua wafanyakazi wawili wa
kampuni ya  Bonite Bottlers Moshi Jumatatu wiki hii.

Wafanyakazi hao wawili wa Bonite Bottlers Moshi,ambayo ni moja ya kampuni za IPP, wakiwa kwenye gari Toyota Hiace ,lenye namba za usajili T 803 ATR,waliuawa na watu wanne wanaodhaniwa kuwa ni majambazi karibu na Kili FM Radio,barabara mpya ya Soweto mjini Moshi mkoa wa Kilimanjaro.

Watu hao walikuwa wamepanda pikipiki mbili mojawapo ikiwa ni aina ya Boxer.

Mauaji hayo ya kinyama yaliyoondoa roho za wafanyakazi  hao  waliokuwa wakitegemewa na kampuni na familia zao yanasikitisha sana na  Mwenyezi  Mungu azilaze roho za marehemu  hao mahali pema peponi.


Wakati uchunguzi wa mauaji hayo unafanywa na Polisi, mtu ye yote mwenye taarifa zozote kuhusu uhalifu hu o  atoe taarifa kituo chochote cha Polisi hapa nchini.

No comments:

Post a Comment