Pages

Sunday, April 19, 2015

Namuoa mpenzi wangu wa Arusha as soon as possible - JUMA NATURE

Mkongwe kwenye muzuki wa kizazi kipya nchini Tanzania Juma Khassim Kiroboto maarufu kama Juma Nature @Sir_Nature amesema Kuwa Siku za karibuni zijazo atamuoa mpenzi wake ambaye anatokea Arusha.
Akifanya mahojiano na @DjHaazu wa @MamboJamboRadio Arusha Tanzania, Juma Nature amesema kuwa amekaa bila mke wa ndoa kwa kipindi Kirefu sana tangu aachane na aliyekuwa mkewe ambaye alibahatika kuzaa mtoto mmoja na yeye aitwaye Furaha na kwa sasa anaamini ni Muda muafaka wakufikia hatua nyingine ya kuitwa baba wa familia. 

Katika mazungumzo hayo @Sir_Nature amesema pia kwamba mwanaye Furaha anaishi na mama yake ila yeye kama baba anamgharamia mwanaye kila kitu ikiwa ni pamoja na shule bora huku akisema kuwa yeye na mzazi mwenzake huyo hawana shida wako sawa japo alipata bwana mwingine na kuolewa.

Katika point nyingine pia Nature amewaomba mashabiki wake wakae tayari kwani karibuni anaachia wimbo wake mpya wenye mahadhi ya Kwaito aliosema utaitwa GUSA UNASE.

No comments:

Post a Comment