Pages

Wednesday, April 8, 2015

Nay Amesema Shamsa siyo Mpenzi wake

Staa wa Bongo Fleva, Elibarik Emmanuel ‘Nay Wa Mitego’amefunguka uhusiano wake na mwigizaji wa filamu za Kibongo,Shamsa Ford baada ya picha kadhaa kuzagaa mtandaoni wakiwa kimahaba wakipigana mabusu.
Akipiga Stori na Clouds Fm alisema kuwa hana uhusiano wa kimapenzi na mwanamke yoyote kwa sasa siyo tu Shamsa Ford, na nafasi ipo kwa yoyote anatakayekubali kuwa mpenzi wake.

‘’Jamani nipo singo kwa sasa sina uhusino na mwanamke yoyote na Shamsa siyo mpenzi wangu,’’alisema Nay. Akizungumzia picha zilizozagaa mtandaoni akipigana mabusu na mwigizaji huyo alisema kuwa hiyo ni filamu yao mpya ya kimapenzi ambayo itatoka muda si mrefu kuanzia sasa.

‘’Ile picha ni vipande vya movie yetu ya kimapenzi mimi na Shamsa bado hatujaipatia jina kwa sasa mashabiki wasubiri tu wataiona halafu Shamsa hawezi kuwa mpenzi wangu kwa sababu ni ndugu yangu ni binamu yangu,’’alisema Nay.


Shamsa naye alipoulizwa kuhusiano na picha hizo alisema ni filamu yao mpya wanafanya.

No comments:

Post a Comment