Pages

Tuesday, April 14, 2015

Nyumba yako inawezekana kuwa imepambwa, safi, nadhifu na maridadi hata kama una watoto wadogo ndani

Wazazi wenye watoto wadogo huwa wananiuliza kama inawezekana kuwa na nyumba iliyopambwa vizuri na kuwa na watoto ndani wakati huohuo. Jibu ninalowapa ni NDIO! Njia nne za kuweza kupamba nyumba yako hata kama unaishi na watoto wadogo ni hizi.

Sehemu kubwa ambayo watoto wanapenda kucheza na kuchafua kwa vyakula na vinywaji ni kwenye sofa. Hata kama utajitahidi kuwazuia namna gani mwishoni hivyo vita mzazi hutaviweza, utashindwa tu, kwani utatoka na kurudi na kukuta wameshamwaga tomato sauce. Suluhisho lake ni weka sofa zenye kitambaa kisichoonyesha uchafu na pia vitambaa vyake viwe ni vya kuvulika kiasi kwamba unaweza kuviondoa na kufua.

Usiweke coffee table ya kioo, weke ya mbao ambayo ncha zake sio kali au kama utapenda nzuri zaidi ni ya kitambaa (ottoman). Coffee table ya kioo ina uwezekano mkubwa wa kuvunjwa na watoto na ikawaumiza vilevile.

Ongeza mapambo kwenye zile sehemu ambazo watoto wako wadogo hawafilkii. Unaweza ukawa na display cabinet lenye mapambo yako ya crystal na kwa vile watoto hawafikii vikakaa vizuri kabisa, badala ya kuviweka juu ya coffee table. Hata picha za ukutani zilizo juu watoto ambao hawajawa na uelewa hawawezi kuzifikia

Watoto wanapenda kuvuta pazia na kujificha nyuma ya pazia. Kwa kufanya hivi wanaweza kuzing’oa na pia kuzichafua. Suluhisho lake ni kuwa ukiwa na watoto wadogo weka pazia fupi, zinazopita dirisha kidogo tu, usiweke zile za kuburuza hadi sakafuni kwa kuwa zitakuwa kishawishi kwao kuzichezea.


Usikose kupita kesho kwa tip nyingine ya nyumbani….upate siri za kufanya makazi yako yaonekane nadhifu. 

No comments:

Post a Comment