Pages

Sunday, April 12, 2015

PICHA: Wachezaji wa Zamani wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Barcelona Wamtembelea Raisi Kikwete Ikulu



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jana, Jumamosi, Aprili 11, 2015, amekutana na wachezaji

nyota wa klabu ya soka la Barcelona ya Hispania katika shughuli iliyofanyika Ikulu, Dar Es Salaam. Wachezaji hao wakiongozwa na nyota wa Barcelona na timu ya taifa ya Uholanzi kwenye Fainali za Kombe la Dunia mwaka 1974 nchini Ujerumani Johann Cruyff pamoja na nyota mwingine wa klabu hiyo na nchi hiyo, Patrick Kluivert wamekaa Ikulu kiasi cha dakika 40 kabla ya kuondoka kwenda Uwanja wa Taifa kwa mchezo wao na nyota wa zamani wa Tanzania.
Chanzo: Vijimambo Blog

No comments:

Post a Comment