POLISI mkoani Kilimanjaro inawashikilia wahamiaji haramu 52
ambao ni raia wa Ethiopia kwa tuhuma za kuingia nchini kinyume cha sheria
wakitokea Kenya kwenda Malawi na baadaye Afrika Kusini.
Wahamiaji hao waliokamatwa jana saa 8.23 za asubuhi
wakati askari wakiwa doria katika eneo la Changbay, barabara kuu ya Moshi ña Arusha
wilayani Moshi, walikuwa raia 44 wa Ethiopia.
Kamanda Polisi mkoani hapa, Geofrey Kamwela, alisema raia
hao walikuwa wakisafirishwa kwenye gari aina ya Fuso lenye namba za usajili
T209 BVL, ambapo lilikuwa limepakia karatasi cha matumizi ya chooni maarufu
kama toilet paper ambalo lilikuwa likiendeshwa na Elisha Manyani (45).
Mtu huyo alikamatwa na wenzake watatu ambao Hamza Ali
(24), Isaya Patrick (25) na Steven Swame(39) wote wakazi wa Arusha.
ìWahamiaji hao walikuwa wamepakizwa kwenye gari aina ya
Fuso, ambapo katika gari hiyo, bodi ilikuwa imegawanywa sehemu mbili nyuma
kulikuwa kumewekwa toilet paper na katikati palikuwa pamewekwa raia hao likiwa
limefungwa turubai, jambo ambalo lilikuwa gumu kubaini kama ndani kuna raia
hao,îalisema Kamwela.
Alisema majira ya 8.45 asubuhi raia wengine wanane
walitiwa mbaroni katika eneo la eneo la KDC kwenye Kata ya Kiboroloni, ambapo
walikutwa wakizagaa katika pori dogo karibu na mto Rau.
Kamanda alisema wanaendelea na uchunguzi na hatua za
kisheria zitachukuliwa dhidi ya watuhumiwa hao.
Hatutawafumbia macho raia hao wa Kitanzania
wanaoshirikiana katika kusafirisha wahamiaji haramu na hatua kali za kisheria
zitachukuliwa na hata kutaifisha mali zao pindi watakapokutwa na hatia,”
alisema.
UHURU ONLINE
No comments:
Post a Comment