Pages

Wednesday, April 22, 2015

WATU 10 WAMEFARIKI KATIKA AJALI ILIYOHUSISHA BASI LA UNIQUE NA LORI LA COCACOLA MKOANI SHINYANGA

Watu kumi wamepoteza maisha katika ajali iliyotokea katika kijiji cha ibingo kata ya Samuye mkoani shinyanga ajali iliyohusisha basi la UNIQUE lenye namba T148BKK na LORY la kampuni ya COCA COLA lenya namba za usajili T207BSA liliokua linakokota tela namba T655AJT.

Kwa maelezo ya abiria aliyenusurika katika ajali hiyo Kevin Moshi ameeleza Dereva wa gari hilo alikua anaendesha kwa mwendo kasi na walipofika katika eneo la Samuye wakakutana na Lory hilo likiwa katikati ya barabara na ndipo ajali ikatokea.

Kwa upande wake kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na amesema watu tisa wamekufa hapo hapo na mtu mmoja amefariki wakati akipelekwa katika hospitali lakini amewataka madereva kuendesha magari kwa kuzingatia sheria za barabara ili kuepusha ajali ambazo zimekua zikigharimu maisha ya watu.

Naye diwani wa kata ya samuye amosi shija amesema alishuhudia ajali hiyo baada ya kusikia kishindo kikubwa lakini basi hilo lilikua katika mwendo mkali hali iliyosababisha ajali kutokea baada Dereva wa basi kushindwa kupishana Lory hilo.

ITV

No comments:

Post a Comment