Pages

Thursday, April 16, 2015

wazowea kufuga majini, sasa yanakugeukieni!!

Kutoka Mzalendo.net
kwa muda mrefu CCM na serikali zake zikiimba kuwa kusichanganywe dini na siasa !! na huku kinyume chake kinalea mfumo kirito.kwa kuamini ndio njia mujaraab ya kujihifadhi na kukomaa na utawala wao wa CCM milele!! walisahau ya kwamba jini hili halikuli likakwisha!! na siku zote jini huwa ana miko yake. killa baada ya muda kama hutoweza kumtimizia jini huyo haja zake atakuadhibu ujijutie.

Kulipodhihiri mfumo kristo Tanzania, na Watanzania kugutuka kuwa mfumo huo unawamaliza, walitanabahi, na kuanza kupiga mayowe kuulalamikia. kwa kuwa majini hayaonekani, ilikuwa ni kosa kutajwa khasa mchana wakati majini huwa wamelala na kujifungia. Ikaonekana kuwa wanaolaumu mfumo huo na Mambo hayo watafutiwe jina nakuwa MAGAIDI, haya yameanza zamani sana, na kuendelea chini kwa chini mpaka kuzoweleka na kutendwa hadharani mchana kweupee kwa kuamini kuwa yameshazoweleka.

Kinyume chake ni kuwa kumezuka MUAMSHO na wenzao kama hao kupiga mayowe na kulalamika juu ya mfumo wa aina hio kuwaathiri kwa hali na mali, na kwa hilo kukazushwa ile dhana yakuwa watu wa aina hio ni MAGAIDI na wanafaa kupigwa vita kwa hali yoyote ili watokomezwe!! Uamsho wakaandamwa usiku na mchana mpaka viongozi wao wakatiwa ndani. na si hayo tu, wakafanyiwa killa aina ya machafu ili kukomesha tabia hii ya kukemea zindiko la jini lao, kwakuamini yakuwa ndio dawa ya kunyamazisha kuhojiwa jini hilo. lakini wapii!! wamesahau yakuwa jini si binaadamu na jini si wa kuaminiwa. anapokosa tambiko lake wakati wowote anaweza kugeuka!!

Sasa mfumo Kristo umewageukia!! unataka kuwatowa kikowa CCM na serikali zake zote mbili, sasa wamebaki kuweweseka ati watamfungia jini hili lisiweze kuendelea kutambika!! huku wakisahau ya kwamba walipokuwa wakimfuga jini hili, walikuwa wakilifukiza udi, sasa udi huo umewaishia wanataka kumfukiza kwa ubani???

Sasa jini hili halikuzowea kufukizwa kwa ubani, na sasa CCm na serikali zake udi umewaishia wafanyajeee??
ati hii leo wanamtishia kumfungia juwani!! kweli atakubali wakati juwa likimmurika linamdhuru jini huyu?

Ati hii leo kunasikika kauli za kutaka kufungia taasisi za kidini ambazo zinaingilia siasa, zilizoasisiwa na wao wenyewe kwa maslaha yao kwa kunyimwa usajili na kuvifunguia!!haya yalisikikana zamani kwa kutaka kuufungia umoja wa Uamsho kwa kuendelea kuwaamsha wananchi kula daku!! wakati hii leo wananchi wameshaamka kwa kelele za MUAMSHO ati hivi sasa ndio wanataka kufunga banda wakati farasi wameshatoka? kwa UAMSHO si kazi kuifungia!! maana wamechanganywa na sifa ya UGAIDI !! lakini hawa mfumo Kristo ambao waliokuwa wakiwafuga kwa miaka nenda miaka rudi, kweli wataweza kuwafungia na kuwanyima vibali na usajili? SUBUTTUUU !!!! hii leooo?

Natusubiri tuone kama CCM na serikali zake zina uwezo huo wa kumfunga jini hili kengele mchana kweupee!!
wakati utatueleza !!


Kidumuuu!!!!!

No comments:

Post a Comment