Pages

Saturday, May 30, 2015

Jinsi ya Kuuteka Moyo wa Mwanamke

lol..hii makala ni ndefu ila hutajututia muda wako kuisoma..tunajifunza kila leo.
KATIKA ulimwengu wa mapenzi, baadhi ya wanaume hujikuta katika wakati mgumu, kutokana na kushindwa kuwashawishi wanawake hata wakawapata kimapenzi, iwe katika mapenzi ya kawaida, au hata uchumba ambao hatima yake ni ndoa. 

Ukweli kuhusiana na suala hili ni kwamba vijana wengi wa siku hizi hawafahamu jinsi ya kukabiliana na wanawake, ama kwa kuwa hawapati mafunzo ya kutosha kutoka kwa wazazi wao, au pengine kutokana na wanawake wa sasa kuwa wajanja, kiasi kwamba wanawatisha na kuwakatisha tamaa mapema.
Ni dhahiri kuwa vijana wengi wa zama hizi huwachukulia wanawake kwa mtazamo fulani ambao hauwasaidii kuwafahamu vema, hali ambayo matokeo yake ni kukosekana kwa mafanikio na tija katika suala la mapenzi. Katika zama hizi ambapo ungangari wa wanaume umepungua kutokana na kampeni za usawa wa jinsia, vijana wa kiume ama huwaona wasichana kama vituo vya polisi, au wengine huwaogopa kutokana na kujidhania kutokuwa na uwezo wa kifedha wa kuwatosheleza, hasa mwanamke anayehusika anapokuwa ni mrembo wa kusemwa na wengi. Unaweza kuwa umezimika au umekufa na kuoza kwa mwanamke, lakini pia ulimi wako ukawa mzito, hata ukashindwa kumweleza haja yako na kumfanya avunjikevunjike na kukupenda, hata kama hakuwa na wazo la kukutana na wewe maishani mwako.

Jambo la muhimu la kwanza ambalo kijana wa kiume hupaswa kulizingatia ni kwamba, unapoanza kutafuta wasichana kwa minajili ya mapenzi, unapaswa kwanza kuwa mtu wa kujiheshimu na kuonesha heshima kwao pia. Baadhi ya watu husema, mheshimu msichana unayemfuatilia, kama ambavyo ungependa kuona mama yako au dada yako akiheshimiwa na mume/bwana wake.

Lakini pia, unapotaka kujiongezea nafasi za kupata mwanamke, hususan kama unataka mmoja tu kwa ajili ya mapenzi ya daima au ndoa, jitahidi kuwa mtafutaji. Simba asiyewinda mwishowe ama hufa njaa, au huishia kula wanyama dhaifu kama binadamu. Usipojihangaisha katika kipindi muafaka cha kutafuta mwanamke unaweza kujikuta ukiwanajisi watoto wasioweza kujitetea na ukaishia jela.

Unapokutana na msichana kwa mara ya kwanza na kuzungumza naye kuhusiana na mapenzi, mwoneshe tabia ambayo atahisi kuwa inakutofautisha na vijana wengine wote wa kiume aliopata kukutana nao kwa mazungumzo, au anaofanya nao kazi ofisini, au anaosoma nao. MTENDEE UUNGWANA, UKARIMU Ili kuhakikisha unaiteka roho ya msichana kwa jinsi hii, jitahidi kuwa mtu wa mahaba, badala ya kuonekana kuwa na tamaa ya kumwingilia kimwili. Pia mshike mkono wake kwa jinsi isiyoonesha tamaa bali upendo, mfungulie mlango wa nyumba na gari, mwandalie kiti mfikapo mahali na mkataka kukaa na kwa ujumla mfanyie ukarimu na uungwana.

MCHUKULIE WA THAMANI Pia katika vitendo vyako, mfanye msichana adhani unamchukulia kuwa wa thamani na wa maana sana . Unapompeleka nyumbani kwako, mathalani, mbusu mkononi au shavuni (akiwa tayari) wakati wa kuagana naye, huku ukimwahidi kuwa utampigia simu. Msichana atashangaa na kujiona wa thamani kubwa kwako, kwani umemtendea kama mtu muhimu kwako. MTENDEE KAMA MALKIA Ikitokea ukatoka na msichana huyo mara nyingine, au akakutembelea nyumbani kwako, endelea kumchukulia kama binti mfalme au binti malkia.

Katika zama hizi za kupungua kwa upendo katika jamii, wanawake wana kiu ya mahaba na mwanaume anayefahamu jinsi ya kutoa mahaba ni mtu adimu kwa watu wa jinsia ya kike. USIHARAKIE NGONO Katika siku za kwanza, hakikisha kuwa huwi na haraka ya kutaka ngono, kwani ukivuta subira, msichana mwenyewe atakuonesha kwa ishara kuwa yuko tayari kwa ngono. Vuta subira, kwani kabla hujakata tamaa na kujiona unachelewa kuonja asali, tayari msichana huyo ataanza kuanguka penzini na wewe kwani wewe ni mwanaume unayemheshimu na kumtendea kwa ukarimu, mahaba na heshima. 

Hakika hata yule mwanamke anayedhaniwa kuwa malaya au changudoa hupenda kutendewa hivi na mwanaume. Kwa hiyo kwa ujumla, kabla ya kufikia mahali ukajidhania kufanikiwa katika medani ya utongozaji na ukampata mwanamke wa kukufaa, unapaswa kufahamu ni nini hasa wanawake hutaka kutoka kwa wanaume na jinsi ya kujipatia nafasi katika moyo wake na baadaye kuuteka.

SIFIA UZURI WAKE Mwambie msichana huyo kuwa ni mzuri, na kwamba ni mtu wa kufaa kuwa naye maishani – mtu anayefaa kuwa mama wa watoto wako. Wanawake hupenda sifa kama hizo hasa kama watahisi kuwa mwanaume amezitoa kwa dhati na si kwa kutania au kudhihaki, au kumvalisha kilemba cha ukoka. Hapa inambidi mwanaume kuwa makini, asije akatia chumvi sana , akashtukiwa. 

ACHANA NA WANAWAKE WENGINE Jambo lingine la muhimu ni kuhakikisha kuwa unapokuwa unamfuatilia mwanamke mmoja huwi na tamaa ya kuwafuatilia wengine wengi. Hakikisha kuwa msichana unayemfukuzia anahisi kuwa umeweka akili yako yote kwake. Hata hivyo, hakikisha kuwa hufikii mahali ukawa kama mjinga kwa ajili ya kutaka kumfurahisha, kwani hakika hutamfurahisha kwa kufanya hivyo bali unaweza kumkosa. 

Na kama baada ya kumtendea ukarimu na kumheshimu bado ataonekana akiendelea kuambatana na wanaume wengine au kuzungumzia wapenzi wake wa zamani, achana naye kwanza, kwani huyo hajakuheshimu. Hakikisha kuwa mwanamke unayemheshimu yeye pia anakuheshimu, la sivyo achana naye na muda si muda watakujia wanawake wakionesha nia ya kukutaka. Usikubali kupoteza nguvu zako na muda wako kwa msichana anayeonesha kila dalili kuwa hakupendi na anakuyeyusha.

MFANYE KUWA RAFIKI Lakini kuna ushauri mkubwa zaidi anaoweza kupewa mwanaume, hasa kijana, kuhusiana na wanawake. Ukiutekeleza ushauri huu basi karibu kila mwanamke utakayekutana naye atakupenda na inaweza hata ikadhaniwa kuwa unatumia dawa. Ushauri wenyewe ni kwamba jitahidi kumfanyia urafiki mwanamke unayetoka naye. Mpe nafasi ya kujisikia huru na salama awapo na wewe na utabaini muda si mrefu kuwa umekuwa mmoja wa wanaume wanaopendwa zaidi katika sayari hii kwani wanawake wengi ( kama si wote) watakupenda. Hii itatokana na ukweli kuwa kila msichana utakayetoka naye, hata katika hali isiyokuwa ya kimapenzi, atawaeleza marafiki zake kuhusiana na tabia yako na kila mmoja atatamani kutoka na wewe kwani unafahamu jinsi ya kumkuna mwanamke pale panapomwasha, kwa matendo yako.

Inaaminika kuwa kitu ambacho humfanya mwanamke ampende sana mumewe au bwana wake, au mwanaume mwingine yeyote, ni ule ukweli kuwa mwanaume huyo amemwonesha urafiki mkubwa. Rafiki ni mtu ambaye mnajuana, kupendana na kuaminiana na mara nyingine huweza kuitwa maswahiba au wandani. Ni mwanamke mjinga tu asiyeweza kumpenda mtu aliyemwonesha sifa hizi. USIJILAZIMISHE KUMPENDA Jambo la msingi kabla ya kutekeleza yote yaliyobainishwa hapo juu ni kujihakikisha wewe mwenyewe kwanza kuwa mwanamke mwenyewe unampenda kwa dhati na si kwamba amekulazimisha mwenyewe kwa kukuganda. 

Hakikisha kuwa hujilazimishi kuambatana na mwanamke ambaye rohoni mwako huhisi kumpenda. Kama msichana atakujia na kukwambia kuwa anakupenda lakini wewe ukawa huhisi mapenzi kwake, kuwa mkweli na kumwambia kuwa hauko tayari kuambatana naye. Wanawake pia humpenda mwanaume aliye muwazi na mkweli. HAKIKISHA ANAKUPENDA KWELI Sasa baada ya jitihada zote za kumwingiza 'line' mwanamke ambaye una uhakika kuwa unampenda, unaweza ukajikuta katika mtihani mwingine: hujui kama mwanamke unayemfukuzia amekupenda kwa dhati au la. Hupaswi kuwa na wasiwasi kuhusiana na hili pia. 

Hebu tuangalie dalili kadhaa za mwanamke ambaye hakupendi. Kwanza, kama mwanamke hakupendi, hata baada ya kumwonesha kila dalili kuwa unamjali na umemfanya swahiba wako, utabaini kuwa kila unapotaka kumkaribia yeye anasogea, au anakukwepa. Mwanamke huyu pia utamwona akionekana kama mtu aliyekerwa na jambo kila unapokutana naye, ataepusha macho yake kukutana na yako, atakunja mikono yake kifuani mwake kuepuka kukushika mkononi mnapokutana na atajitahidi kufunga miguu yake unapozungumza naye. Pia mwanamke huyu ukiwa naye anaonekana kutojali na kama ana simu atakuwa anatuma au kupokea ujumbe wakati wewe ukimweleza jambo. 

Tena wakati ukizungumza naye utabaini kuwa macho yake yameelekezwa kwa wanaume wengine kama wapo – ishara kwamba katika wewe bado hajampata mwanamume anayemfaa. Mwanamke huyu pia hatafanya jitihada za makusudi za kutaka kuzungumza na wewe, utamsifia lakini hatajibu, wala hatajibu maswali yako na hatauliza maswali yoyote kuhusiana na wewe au mambo yako. Kama msichana huyu haumwi, basi dalili hizi zinatosha kukufahamisha kuwa hakutaki na ukiendelea kumfuatafuata unaweza kujikuta unapoteza muda wako bure. 

Mwanaume mwenye hekima hufahamu maana ya dalili hizi na hasubiri mwanamke amtamkie kuwa 'sikutaki' au kumtukana na kumdhalilisha hadharani. Kama Waswahili wasemavyo, mara nyingi akufukuzaye hakwambii toka. Pamoja na kwamba zipo sababu nyingi binafsi za mwanamke kutojisikia kumpenda mwanaume, yawezekana sana kuwa katika uchunguzi wake amebaini kuwa wewe si mtu wa mahaba na kwamba huwezi kuwa mwandani wake wa maisha, au pengine amekushtukia kuwa unamfuatilia mwanamke mwingine. Ili kuepuka adha ya kunyanyaswa na mwanamke kwa kukataliwa, unapaswa kuzifahamu sifa kadhaa anazopaswa kuwa nazo mwanaume ili kuishinda roho ya kigumu ya mwanamke. 

Kwanza, mwanaume mwenye uwezo wa kuiteka roho ya mwanamke ni yule ambaye anapoingia katika mbio za kutafuta mpenzi au mchumba hufahamu anachokifanya, huku akijua kuwa hakuna muda wa kupoteza.

Huyu huchukua hatua kuhakikisha anavuta hisia za mwanamke. Pili, mwanaume mshindi katika fani hii ni yule anayejifunza kutokana na mafanikio yake ya zamani na kusahau kushindwa kwake kwa zamani. Mwanaume huyu huzingatia kuboresha upande wake, akiboresha mwonekano wake na tabia zake, ili kumvutia mwanamke. Vilevile, mwanaume mshindi katika medani ya mapenzi huwa mtu wa kujiamini. Hujisikia yuko huru na salama mbele ya wanawake, jambo ambalo wanawake hulichukulia kama sifa mojawapo ya mwanaume wa kufaa. Pia mwanaume mshindi huifahamu siri ya kufurahi na kila apatapo muda mzuri huonesha furaha na tabasamu. Mwanaume huyu hufahamu jinsi tabasamu, kicheko na bashasha vinavyoweza kumvutia mwanamke na kuuvunjavunja moyo wake.

Mwanaume aliyeifahamu siri ya ushindi katika mapenzi pia si mtu wa kusitasita, bali kila anapoona upenyo wa kumfikia mwanamke amtakaye huutumia, bila kuanza kufikiria jinsi ya kuanza, wala matokeo. Mwanaume huyu hufahamu kuwa wajibu wake ni kuomba na kwamba suala la kunyimwa au kupewa ni la mwanamke. Kuna usemi wa kabila moja hapa nchini usemao 'mwombaji haaibiki, bali huaibika anayemnyima'. Nadhani wanaume hawa huuzingatia usemi huu pia. Pia mwanaume mwenye uwezo wa kuiteka roho ya mwanamke ni yule ambaye hujiwajibisha kwa asilimia 100 katika jambo lolote linaloweza kutokea katika maisha ya kimapenzi. Mwanaume huyu hujiona anahusika, bila kujali kuwa jambo lililotokea ni zuri au baya. Mwanaume huyu hajengi msimamo wake kutokana na kushindwa kwake kumpata mwanamke fulani, bali hujifunza kutokana na kila kosa. Pia huwa na mawazo chanya, mathalani aendapo kwenye mtoko huzingatia tu kuwa anakwenda kuburudika, bila kujali kuwa linaweza kutokea jambo baya huko. 

Hizo ni baadhi tu ya sifa za 'mabingwa' katika suala zima la mapenzi. Kama utazifanya kuwa sehemu ya hulka yako, ni wazi kuwa utafanikiwa sana katika mbio zako za kumtafuta mpenzi na hutakuwa na maswali mengi kuhusu iwapo mwanamke amekupenda au la, kwani kila kitu kitakuwa dhahiri. Ushauri: 0654 043953

No comments:

Post a Comment