Pages

Tuesday, May 12, 2015

Kajala anaendelea vizuri baada ya kupigwa na chupa usoni..

Staa wa Bongo Movies, Kajala Masanja anaendelea vizuri baada yakupigwa chupa na kijana mmoja usiku ya kuamkia jana wakiwa kwenye show ya mwanamziki Mabeste aliyoiandaa ili kuchangisha pesa kwa ajili ajili ya matibabu ya Mkeo.
Leo kupitia ukurasa wake mtandaoni, kajala ameweka picha hiyo hapo juu  na kuandika  “Maisha yanaendelea au sio......” kuonyesha kuwa yupo poa na anaendelea na masiha yake yakawida.

Akilezea tukio hilo la kupigwa na chupa hapo jana alipofanya mahojiano na mtangazaji Millard Ayo wa Clouds FM kajala alieleza

“Mpaka tumemaliza show, sasa kwenye muda wa kuondoka nikamwambia Meneja wangu amuite msanii wetu mmoja anaitwa Tausi ili tuondoke, sasa wakati nataka kushuka kwenye gari natembea tu sijui chochote nikashangaa chupa imenipiga usoni, nikadondoka na kubiringita kwenye zile ngazi, kuna mkaka na mdada wakaniona wakanisaidia”

Akaongeza kuwa;

 “Aliyenipiga na hiyo chupa ni Mwanaume, simjui na wala sijawahi kumuona hata mara moja…. amekamatwa yuko Osterbay Polisi, nilivyotoka Maisha Club nilipelekwa Hospitali Mwananyamala nimeshonwa usoni aliponiumiza, tukarudi Polisi nikaandika maelezo”.

Pole sana Kajala


BONGOMOVIES

No comments:

Post a Comment