Pages

Wednesday, May 13, 2015

KEISHA: Nahitaji kulea madume yangu..

BAADA ya mashabiki wake kumtaka aongeze mtoto wa tatu, msanii wa Bongo Fleva, Khadija Shaban (Keisha), ameibuka na kuweka wazi kwamba hana mpango wa kuzaa tena kwa sasa.

Keisha aliliambia MTANZANIA kuwa, sababu kubwa inayomfanya asitamani kuongeza mtoto kwa sasa ni kutokana na kuwa na watoto wawili wa kiume wenye umri mdogo.

“Najua watu wengi wanapenda watoto na hata mashabiki wangu wanatamani sana niendelee kuzaa, kiukweli bado nahitaji kulea madume yangu, kwani umri wao bado ni mdogo sana,” alisema Keisha.

Mtoto wa kwanza wa msanii huyo ana miaka minne na wa pili ana mwaka mmoja.


“Kama nitabeba ujauzito mwingine kwa sasa mimi na baba yao tutakuwa hatuwatendei haki hawa watoto wetu, wanahitaji muda wa kukua zaidi ndipo tufikirie kuongeza wenzao wengine,” alisema Keisha.

No comments:

Post a Comment