Pages

Tuesday, May 19, 2015

Khadija Kopa hataki waonyesha vifua kwenye bendi yake mpya ya Kopa Kopa

MALKIA wa mipasho nchini Tanzania, Khadija Kopa, ameweka wazi wasanii anaowataka katika bendi yake ya Kopa Kopa huku akiwaponda wanaovua nguo stejini kwa ajili ya kuonyesha vifua vyao.

Mkali huyo wa mipasho anayetarajia kufanya ‘remix’ ya wimbo wa ‘Nipepee’ na msanii, Abdul Nassib ‘Diamond’, aliliambia MTANZANIA kwamba hapendi kuwa na wasanii wanaoonyesha vifua vyao kwa kuwa bendi yake inaheshimu maadili ya Tanzania.

“Wasanii wanaovua nguo jukwaani kwa ajili ya kuonyesha vifua vyao kwa sababu zao binafsi hawana nafasi katika bendi yangu ninayotaraji kuizindua hivi karibuni kwa ajili ya burudani kwa Watanzania wote,” alisema Kopa.

Kopa aliongeza kwamba, kwa sasa yupo katika mazungumzo na kiongozi wa kundi la TMK Family, Said Fella kwa sababu ya kushirikiana nao.


“Nazungumza na Fella ili niweze kufanya uzinduzi, lakini pia nataka anisaidie niweze kufanya shoo za nje na bendi yangu kwa kuwa licha ya kutamba nchini nataka kujitanua zaidi kwa soko la nje kama wafanyavyo baadhi ya wasanii wa Bongo Fleva,” alifafanua Kopa.

No comments:

Post a Comment