Pages

Tuesday, May 5, 2015

Lady Jaydee sio mkikuyu


MWANAMUZIKI Judith Wambura ‘Lady Jay Dee’, ameweka wazi kwamba yeye ni Mtanzania na si Mkikuyu kutoka Kenya kama baadhi ya mashabiki wa muziki kutoka nchini humo wanavyomdhania.

Jay Dee ameeleza hayo baada ya kudai kwamba kila anapokuwa katika maonyesho yake ya muziki nchini humo, mashabiki wake humtaka ahamie nchini humo moja kwa moja.

“Unajua Wakenya wamekuwa wakisema mimi ni Mkikuyu, wanadai natakiwa nikaishi nchini kwao wanajua mi ni Mkikuyu ila nawaeleza ukweli ni kwamba naipenda Kenya, lakini mimi ni Mtanzania na daima nitaipenda nchi yangu,” alifafanua Jay Dee.

Hata hivyo, katika hatua nyingine mwanadada huyo anajiandaa kushirikiana kwa mara nyingine katika wimbo wake mpya na msanii kutoka Burundi, Kidumu, ambaye awali walishatoa wimbo unaotambulika kwa jina la ‘Nitafanya’.

MTANZANIA

No comments:

Post a Comment