Pages

Sunday, May 31, 2015

Lowassa Atangaza Nia ya Kugombea Uraisi

Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa ambaye pia ni waziri mkuu wa zamani wa Tanzania, akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea ofisi ya CCM mkoa wa Arusha. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Arusha, Bw.Onesmo Ole Nangole.
Kinyang’anyiro kwa kuwania uteuzi wa kugombea urais kwa tiketi ya chama tawala cha CCM nchini Tanzania, kimepamba moto  kwa  kwa staili ya aina yake .

Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa ambaye pia ni waziri mkuu wa zamani wa Tanzania Jumamosi amejitokeza
mbele ya umati wa wanachama na wafuasi wake katika uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kuelezea kuwa ataomba uteuzi wa chama tawala kuwania urais katika uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.

Bw. Lowassa ni miongoni mwa wanachama kadhaa wa chama tawala ambao wameelezea nia yao ya kuomba utezi wa chama tawala ili kushiriki katika kinyang’anyiro cha urais mwaka huu. 

Baadhi ya wanachama wengine wa CCM ambao wametangaza nia ya kutaka kuwania urais wa Tanzania ni pamoja na MBalozi wa Umoja wa Afrika hapa nchini Marekani, Amina Salum Ali ambaye aliwahidi kuwa waziri wa fedha wa Tanzania. 

Siku chache zilizopita Balozi Amina alitangaza kuwa anaingia katika mbio hizo za kuwania uteuzi wa chama tawala.

VOA

No comments:

Post a Comment