Pages

Monday, May 11, 2015

Machafuko nchini Burundi.....Nyumba zinazowindwa zadaiwa kupakwa rangi nyekundu..

Mfano wa nyumba ya rangi nyekundu
WAKIMBIZI wanaokimbia vurugu zinazozidi kuongezeka nchini Burundi wamesema kuwa, wajumbe wa kitengo cha vijana wa chama kinachoongoza serikali nchini humo wanapaka rangi nyekundu katika nyumba za
watu wanaowindwa, wakala wa wakimbiza wa Umoja wa Mataifa (UN) umekaririwa mwishoni mwa wiki na Shirika la Habari Uingereza (Reuters) na kuripotiwa jana.

Kulingana na taarifa jana, pia kuna ripoti za watu wanaouza mali zao kabla ya kuondoka katika nchi hiyo, hali inayoelekea kwamba hawategemei usalama wao kwa muda mrefu.
Zaidi ya Warundi 50,000-wengi wao wakiwa wanawake na watotowamekimbilia nchi jirani katika wiki za karibuni kutokana na vurugu hizo zilizochochewa na mpango wa Rais Pierre Nkurunziza wa nchi hiyo kugombea tena nafasi hiyo kwa mara
ya tatu.

Wapinzani wamekaririwa kuwa, hatua hiyo inakiuka katiba ya nchi hiyo pamoja na mpango wa amani ambao ulikomesha vita vya kikabila vya mwaka 2005.

Vurugu hizi zimezuka katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati ambako hali inasadikiwa kuwa mbaya tangu vita ya miaka 12 ambayo ilizaa waasi kutoka katika Kabila la Wahutu walio wengi dhidi ya jeshi lililokuwa likiongozwa
na Watutsi ambapo, watu 300,000 waliuawa.

Shuhuda mmoja aliyetajwa kwa jina la Edwards ambaye haikuelezwa ni nani ameileza Reuters kuwa, wakimbizi waliowasili nchini Rwanda wameelezea kuhusu manyanyaso na vitisho walivyofanyiwa na wajumbe wa vijana wa Imbonerakure "ambao wanapaka rangi nyekundu katika nyumba za watu wanaowindwa."

"Baadhi waliamua kuondoka kama hatua ya tahadhari, kutokana na kuwahi kukumbana na vurugu za zamani," alinukuliwa akizungumza jijini Geneva, Uswisi.

Chama kinachoongoza serikali cha CNDD-FDD kimekanusha madai hayo kuwa, vijana wake wamepewa silaha na wanajaribu kuchochea vurugu. Kimesema kuwa, wapinzani wao ndiyo wanaojaribu kuongeza msongo.

Edwards alisema kwamba, wakimbizi wanaokimbia wamekuwa wakikabiliwa na hatari nyingi.
"Baadhi ya wanawake wameripoti vitisho vya kubakwa kutoka kwa wanaume wenye silaha na wanalazimishwa kutoa hongo ili
waweze kupita katika vizuizi.
Baadhi wametembea kwa saa kadhaa kupitia
porini wakiwa na watoto wao," alinukuliwa.

Wakala wa wakimbizi imesema kuwa, wakimbizi wengi walitoka Kaskazini ya nchi hiyo, lakini wiki hii ilianza kushuhudia wengine wakiwasili kutokea mijini ikiwa ni pamoja na shule za juu na wanafunzi wa vyuo vikuu.

MAJIRA

No comments:

Post a Comment