Pages

Wednesday, May 6, 2015

Mkurugenzi atoa tuzo ya bahasha tupu......Mchakato wa kupata pesa unaendelea

CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU), wilaya ya Kilolo, mkoani Iringa, kimeendelea kuitikisa halmashauri ya wilaya hiyo kikimtuhumu mkurugenzi wake kutoa zawadi ya bahasha tupu kwa watumishi wake 16 bora wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi duniani, Mei Mosi.
Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya chama hicho kuibua kile walichoita kashfa ya matumizi mabaya ya fedha za halmashauri hiyo yaliyofanywa na maofisa waliohusika na uandaaji na uwasilishaji wa mpango wa bajeti ya mwaka 2015/2016 jijini Dar es Salaam.

Taarifa ya Talgwu ambayo pia imethibitishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Ubald Wampembe, jeshi la Polisi limeanza kuchunguza tuhuma hiyo ya matumizi ya zaidi ya Sh milioni 40 yaliyofanywa kwa maofisa hao.

Akizungumza na wanahabari jana, Mwenyekiti wa Talgwu wa wilaya hiyo, Andrea Mwandimbile alisema katika maadhimisho hayo yaliyofanyika Ilula, wilayani humo, wafanyakazi hao walikuwa wapate zawadi ya kati ya Sh 250,000 na Sh 200,000 kwa kuwa watendaji bora katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.Lakini walipewa bahasha tupu.

Akijibu malalamiko hayo, Kaimu Mkurugenzi huyo alisema; “kulikuwepo na tatizo dogo la mawasiliano lililochelewesha mchakato wa utoaji wa fedha kwa ajili ya kuwapa zawadi watumishi hao.”

Wampembe alisema mchakato wa kupata fedha hizo unaendelea kufanywa na wakati wowote kuanzia sasa watumishi hao watapewa haki yao.

HABARI LEO

No comments:

Post a Comment