Pages

Saturday, May 16, 2015

Nyumba Lulu aliyomzawadia mama yake hajahongwa.....Aliijenga mwenyewe

Mwanzoni mwa mwaka huu (2015) mrembo na muigizaji wa filamu, Elizabeth “Lulu” Michael aliwa-surprise watu wengi pale alipomzawadia mama yake nyumba aliyojenga Kimara, jijini Dar es- Salaam.

Lulu alimpa zawadi hiyo mama yake kwenye sherehe ya siku yake ya kuzaliwa January, 2015. Je Lulu aliwezaje kufanya mambo makubwa kama hayo katika umri mdogo na kwa kipato cha kuigiza peke yake? Hayo ni maswali ambayo wengi walijiuliza, kiasi cha kuwafanya wengine waamini kuwa labda amehongwa.

Lulu amesema kuwa nyumba hiyo alianza kuijenga kidogo kidogo miaka minne iliyopita kwa kile alichokuwa anakipata kupitia kazi yake ya uigizaji, lakini watu wengi hawakufahamu mpaka siku alipoitoa kama zawadi kwa mama yake.

“Kiukweli ile nyumba nimeanza kujenga nikiwa bado mdogo sana, ni nyumba ya chini ya kawaida lakini nilikuwa najenga kidogo kidogo, kwamba leo nikipata laki nampa mama leo kaongezee hiki…kwahiyo ni kwasababu mtu hajui atashangaa Lulu kapata wapi hela za vuuup, lakini ni kitu ambacho kimeenda kidogo kidogo imechukua hata miaka minne..kwahiyo mtu atashtuka kwasababu ameiskia leo sasa ndo hivyo mtu ataanza kusema kahongwa hajui background.” alisema Lulu kupitia The Sporah Show.


Vijimambo

No comments:

Post a Comment