Pages

Saturday, May 16, 2015

PICHA: Laptop za wizi..

Na: Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi DodomaJeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia mtu mmoja aliyekamatwa katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Yarabi Salama (Yarabi Salama guest house) katika Manispaa ya Dodoma. 

Aliyekamatwa anafahamika kwa jina la MASAGARA
S/O MESO, Mwenye miaka 40, Kabila Mzanaki wa Butihama, akiwa na funguo bandia 19, Master key 2, Bisibisi 2, Kisu kimoja, Tupa moja, Mikasi mitatu mikubwa ya kukatia vyuma, Msumeno ya kukatia vyuma mitano, Mitalimbo ya kuvunjia miwili, Adjustable spanner 1, Kipande cha bomba, Biti za kutobolea vyuma na mbao 8, Simu mbili aina ya Tecno na Nokia, Simu ya bandia ya Nokia, Pochi za mfukoni mbili, Hati ya dharura ya kusafiria, Betri ya simu moja, Nyenzo moja ya mbao, Nguo za kubadilisha, Madawa mbalimbali ya kienyeji, Kipande cha nondo kimoja na Irizi moja aliyokuwa amefunga sehemu ya juu ya mkono wa kushoto akiwa amehifadhi kwenye begi lake kwa maandalizi ya kufungua vyumba vya wapangaji wengine na kuvunja mita ili aibe.

No comments:

Post a Comment